Wewee hayo mambo ya Afya ya Akili mara Emotional Intelligence ooh sijui therapy waachie wazungu sio huku kwetu!!

Hapa ni kazi kwenda mbele, mambo ya hisia peleka kwenu!!
Wanaume huwa hawalii hayo mambo ya wanawake, we jikaze tu!!

Ni kawaida sana kusikia mitazamo na maneno kama haya kwenye maisha yetu ya kila siku. Jambo linalo onyesha dhahiri kwamba; Afya ya Akili na Akili Hisia ni mambo ambayo bado uelewa wake uko chini sana kwenye jamii yetu na kwa tamaduni zetu ni mambo ambayo hayapewi kipaumbele.

Hili haliondoi ukweli kwamba wapo wengi kwenye jamii yetu wanao athirika na kutaabika na changamoto za Afya ya Akili. Pia halibadilishi ukweli kwamba Akili Hisia ni njia muhimu sana ya kutawala hisia zetu inayopelekea kustawisha afya zetu kiakili na kuimarisha ufanisi ama uzalishaji wetu kikazi.

Kupitia Emotional Me; Explorer In Chief anaweka sawa nadharia potofu kuhusu Afya ya Akili na Akili Hisia huku akitoa elimu na taarifa sahihi juu ya mambo mbalimbali kuhusu Afya ya Akili na Akili Hisia.

Karibu tusafiri pamoja tukitembelea vituo mbalimbali na kujifunza mengi kwenye ulimwengu wa Hisia.

by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 10, 2025
by Peter Thadeo | Jan 11, 2024
by Peter Thadeo | Jan 11, 2024

Pages